Kituo cha umoja wa utafiti "Future rural Africa" inashirikiana na washirika wengine wanachunguza utayari wa watu wa Afrika Mashariki kulipia chanjo ya COVID 19 inayotarajiwa. Kwa kusudi hilo, unakaribishwa kujibu utafiti huu.
Karibu kwenye utafiti huu
Lengo la utafiti huu: Kituo cha umoja wa utafiti "Future rural Africa" inashirikiana na washirika wengine, Chuo Kikuu cha Gondar (Ethiopia), Chuo Kikuu cha Kabale na Apata Insights (Uganda), Chuo Kikuu cha Bonn (German), Chuo cha New South Wales (Australia) na Chuo Kikuu cha Leiden (Netherlands) wanachunguza utayari wa watu wa Afrika Mashariki kulipia chanjo ya COVID 19 inayotarajiwa. Kwa kusudi hilo, unakaribishwa kujibu utafiti huu. Unapaswa kuwa na miaka 18 au zaidi kushiriki.
Matarajio: Utafiti huu utachukua chini ya dakika 10 kumalizika. Kwanza,utafiti huu utauliza taarifa za msailiwa kama umri, jinsia, kiwango cha elimu na kazi. Pia utafiti huu utatathmini namna COVID 19 imeweza kuathiri kipato chako, kiwango chako cha imani kwa huduma za afya katika nchi yako, na upatikanaji wa huduma za afya kwa sasa.
Utafiti huu pia utachunguza utayari wako wa kulipia chanjo ya COVID 19 inayotarajiwa, iwapo itapatikana kwenye masoko ya ndani kati ya mengine. Utafiti huu utakua katika lugha nne (Kiingereza, Kiswahili, Kiamhariki na Kinyarwanda). Unakaribishwa kujibu maswali kwa lugha yako ya urahisi. Tafadhali soma maswali kwa umakini na ujibu kwa uaminifu.
Kanusho: Hukuna mtafiti au taasisi zao zinahusika katika utayarishwaji wa chanjo ya COVID-19. Watafiti hawashirikiani kwa namna yoyote na makampuni yanayohusishwa na utengenezaji wa chanjo ya COVID-19. Zoezi hili ni kwa maslahi ya utafiti na haichangamani na mipango inayoendelea ya chanjo ya COVID-19. Maoni ambayo yatatolewa katika machapisho kupitia utafiti huu yatakua ya mwandishi tu na hayatawakilisha taasisi zao.
- Kwa taarifa kuhusu mipango ya chanjo ya COVID-19 tafadhali tembelea tovuti ya Shirika la Afya Duniani kupitia here
- Kwa taarifa kuhusu kuzuia COVID 19,tafadhali tembelea tovuti ya Shirika la Afya Duniani here au Vituo vya udhibiti wa magonjwa here